Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza


Jeshi la polisi mkoa wa mwanza linawashikilia watu watano kwa  tuhuma za makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo mauaji.

Tukio la kwanza.

Huko maeneo ya bar ya calfornia, kata ya ibisabageni, wilaya ya  sengerema, jeshi la polisi limewakamata na kuwahoji watu wawili  kwa tuhuma za kosa la mauaji ya zacharia mussa, miaka 26, msukuma, mkulima, mnadani yaliyotokea tarehe 21.02.2021 majira ya  23:30 hrs. Inadaiwa chanzo cha mauaji hayo ni ugonvi uliotokana na  wivu wa kimapenzi ambapo watuhumiwa hao walimjeruhi kwa kitu  chenye ncha kali na baadae akapoteza maisha. Wanahojiwa kwa  kina na mfumo wa kisheria utafuatwa ili kufikishwa mahakamani.

Tukio la pili
Tarehe 22/02/2021 majira ya 03:00hrs huko maeneo ya magela, kata ya  buhongwa, wilaya ya nyamagana, watu watatu wamekamatwa kwa  tuhuma za kumjeruhi hamidu kamugisha, miaka 22, mhaya, mkulima  na mkazi wa buhongwa. Kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali  ubavu wa kushoto. Chanzo cha tukio hili ni ugomvi uliotokana na  pesa walizokua wakidaiana.

Watuhumiwa wa kujeruhi ni:-
    Jackson lucas, miaka 19, muha, mkulima wa buhongwa. Na  wenzake wawili.

Tukio la tatu
Tarehe 20/02/2021 majira ya 13:30hrs huko kituo cha mabasi buzuruga,  wilaya ya nyamagana, askari polisi wakiwa doria walifanikiwa kukamata bhangi yenye uzito wa kilogramu 200 ambayo  ilitelekezwa na watuhumiwa baada ya kubaini wanafuatiliwa. Watu  hao watakamatwa na watafikishwa mahakamani.

Jeshi la polisi mkoa wa mwanza linaendelea na msako mkali katika  maeneo yote, majini na nchi kavu kwenye mitaa, kata na vijiji ili  kuweza kubaini na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na  vitendo vya kihalifu. Pia linatoa wito kwa wananchi pindi  wanapokua na migogoro ya kifamilia wasijichukulie sheria mkononi  bali wafuate taratibu za kisheria na washirikishe taasisi nyingine  zikiwemo za dini kwa utatuzi mzuri wa migogoro hiyo.

Imetolewa na;

Muliro J. Muliro- ACP
Kamanda wa polisi (m) Mwanza.
24 februari, 2021.


from MPEKUZI

Comments