Gavana mstaafu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Benno Ndullu afariki Dunia

 Gavana mstaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu (71) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Februari 22 katika hospitali ya Hubert Kairuki Memorial University alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Katibu muhtasi wake, Msafiri Nampesya ametibitisha kuhusu kifo hicho akisema bado wanafamilia na BoT wanajadiliana kuhusu mazishi yake.

Profesa Ndullu alikuwa Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, kuanzia 2008 hadi 2018 na pia aliwahi kuwa mhadhiri wa uchumi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam.



from MPEKUZI

Comments