Rais Dkt. John Magufuli Jumatano Januari 27, 2021 anatarajiwa kuzindua shamba la miti Chato lenye ukubwa na hekta elfu 69.
Shamba hilo la pili kwa ukubwa katika mashamba yanayomilikiwa na Serikali lipo wilayani Chato, mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amewaambia waandishi wa habari mkoani humo kuwa Rais Magufuli atazindua shamba hilo mapema kesho.
Akielezea manufaaa ya shamba hilo, Mhandisi Gabriel amesema ni matunda ya jitihada za Serikali ya awamu ya tano ya kuhifadhi na kuinua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali za misitu.
“Mradi huu mkubwa wa upandaji miti ambao Serikali imewekeza katika shamba hili unatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika sekta mbalimbali hapa nchini,” amesema Mhandisi Gabriel.
Shughuli ya upandaji miti katika shamba hilo jipya la Chato ilianza mwaka 2018 na pia ni miongoni mwa mashamba 23 yanayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment