NA TIGANYA VINCENT, RS TABORA
NAIBU Waziri wa Elimu , Sayansi na Tekonolojia Omary Kipanga amevunja Kamati ya Ujenzi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi cha Wilayani Uyui na kumsimisha Afisa Ugavi baada ya kubaini mapungufu mbalimbali ambayo yasababisha baadhi ya majengo kuwa na mapungufu.
Pia Naibu Waziri huyo amemsimamisha fundi wa Jengo la Utawala , Msimamizi wa Mradi kwa kushindwa kutafisri sahihi michoro ya ujenzi ambayo imesababisha baadhi ya kutwa kupinda na tofali kujengwa kwa kusimamishwa baada ya kulazwa kama inavyotakiwa .
Kipanga alitoa kauli hiyo jana Wilayani Uyui baada ya kukagua ujenzi wa Chuo hicho ambao umefikia asilimia 23 na kubaini mapungufu katika baadhi ya majengo ambayo yanaendelea kujengwa na yale yaliyokamilika.
Alisema eneo la mradi halivuti kwa kuwa kuna mapungufu makubwa ambayo yameonekana kama vile hakuna mpango kazi unaonyesha kazi zinazofanyika na zinatarajia kumalizika lini, kutokuwepo kwa mpango wa manunuzi unayoonyesha kinachofanyika katika eneo la mradi.
Kipanga alisema mapungufu mengine kuwepo kwa majengo ambayo hayana mafundi na mengine kazi imefanyika lakini yamekosewa.
Katika kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza aliaagiza atafutwe fundi mwingine mwenye ujunzi atakayerekebisha mapungufu katika Jengo la Utawala na kulikamilisha kwa viwango vinavyotakiwa na kuagiza ukuta uliokosewa ubomolewe na kujngwa upya kwa kuzingatia matakwa ya michoro.
Kipanga alisema Mkurugenzi wa VETA kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Tabora kuhakikisha wanaunda Kamati mpya ya ujenzi na kutafuta msimamizi mwenye taaluma ya ujenzi atakayeweza kusimamia vizuri maradi kwa kuzingatia michoro ya majengo.
Aliongeza Kamati ya Ujenzi itakayoundwa ni lazima iwe na wataalamu walau wachache wenye taaluma ya ujenzi ambao watakaoweza kutembelea mara kwa mara mradi na watakaoweza kutoa tathimini ya kweli ya kazi iliyofanyika.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo wa Elimu ameagiza Msimamizi kutoka Chuo cha Ufundi Arusha anayesimamia wa ujenzi na ukarabati wa majengo Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mwanahala wilayani Nzega kuondoka katika eneo la mradi baada ya kushindwa kusimamiwa kazi kwa kuzingatia matakwa ya ramani.
Alisema hataki kuendelea na kazi kwa kuwa ameshindwa kusimamia na kusababisha mafundi kujengea nondo ambazo ni za viwango vya chini ya matakwa yam choro na hivyo kuwa hatari kwa usalama wa majengo.
Kipanga alisema Msimamizi Mshauri anatakiwa kuleta mtaalamu mwingine mwenye ujuzi ambaye ataweza kutafsiri michoro kwa usahihi na kukujenga majengo yanayolingana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.
Wakati huo huo Naibu Waziri huyo alisema kuwa Serikali inatumia zaidi ya shilingi bilioni 56.7 kwa ajili ya ujenzi wa Vyuo vipya vya VETA na kukarabati vyuo vya maendeleo ya jamii(FDC) hapa nchini.
Alisema ujenzi huyo vyuo vipya vya VETA unafanyika katika Halmshauri 29 na kukarabati na kujenga majengo katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii 54.
Kipanga aliongeza kuwa lengo ni kuhakikisha kila kijana ambaye atakuwa amemaliza elimu ya msingi na wale waliomaliza elimu ya Sekondari ambao watakuwa hajabahati kuendelea katika ngazi zinazofuata kupata ujuzi utakaowasaidia kujiari na kushiriki katika ujenzi wa Taifa.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment