Uchumi wa China 'kuupiku ule wa Marekani kufikia 2028'


KITUO cha kutafiti uchumi na biashara kilicho na makao yake huko Uingereza CEBR kimesema kuwa Uchumi wa  taifa la China utaupiku ule wa Marekani kufikia 2028, miaka mitano mapema ya ilivyokadiriwa ripoti.

Wakati huohuo India inatarajiwa kuwa taifa la tatu lenye uchumi mkubwa duniani kufikia 2030.

Kituo hicho cha CBR hutoa matokeo ya utafiti wake kila mwaka tarehe 26 mwezi Disemba.

Ijapokuwa China ilikuwa nchi ya kwanza kuathiriwa na mlipuko wa virusi vya corona , ilifanikiwa kuudhibiti ugonjwa huo kupitia vitendo vyenye masharti makali ikimaanisha kwamba haikulazimika kusitisha kufunga baadhi ya maeneo na kufungua kama inavyofanyika barani Ulaya.

Kutokana na hilo ikilinganishwa na mataifa mengine yenye uchumi mkubwa , imefanikiwa kuzuia mfumuko wa kiuchumi mwaka 2020 na badala yake taifa hilo linatarajiwa kukua kwa asilimia 2 mwaka huu.

Uchumi wa Marekani umeathiriwa vibaya na virusi vya corona kulingana na takwimu. Zaidi ya watu 300,000 wamefariki nchini humo huku takriban watu milioni 18.5 wakiambukizwa .

Ripoti hiyo inasema kwamba baada ya kuimarika kufuatia kuisha kwa virusi vya Covid 19 , uchumi wa Marekani utakuwa kwa asilimia 1.9 kila mwaka kutoka 2022-24 na baadaye kupunguza kasi kwa asilimia 1.6% katika miaka itakayofuata.

Kwa upande mwingine uchumi wa Wachina umedhamiriwa kukua kwa 5.7% kila mwaka hadi 2025, na 4.5% kila mwaka kutoka 2026-2030.

 

Credit: BBC



from MPEKUZI

Comments