Wanafunzi kumi bora Matokeo darasa la 7

Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), limetangaza watahiniwa kumi bora Kitaifa katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi uliofanyika tarehe 7 na 8 Oktoba 2020.
 

Matokeo hayo, yametengazwa leo Jumamosi tarehe 21 Novemba 2020 na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde ambayo yanaonyesha watahiniwa 833,672 kati ya 1,008,307 waliotunukiwa matokeo wamefaulu.

Dk. Msonde amesema, watahiniwa hao wamepata alama 100 au zaidi kati ya 250.

“Idadi hii ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 82.68. Kati ya hao wasichana ni 430,755 ambao ni sawa na asilimia 82.24 na wavulana ni 402,917 sawa na asilimia 83.15,” amesema Dk. Msonde.

Haya hapa majina ya wanafunzi, shule na mikoa. Pia, kuna mgawanyo wa wavulana kumi bora na wasichana.

 



from MPEKUZI

Comments