Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali nchini, Vodacom Tanzania PLC, kwa kushirikiana na Infinix leo imetambulisha rasmi simu mpya aina ya Infinix NOTE 8. Simu hii mpya itaambatana na ofa ya GB 96 za internet kutoka Vodacom Tanzania PLC kwa Mwaka mzima.
Simu ya Infinix NOTE 8 ni ya kwanza toka kampuni hiyo, kuundwa ikiwa na processor ya MediaTek Helio G80 Octa Core, ambayo imetengezwa mahususi kuhakikisha kwa mba mashine inafanya kazi muda mrefu na kwa uwezo madhubuti, na hii ni kuifanya kuwa simu yenye uwezo mkubwa kuliko matoleo mengine ya mwanzo toka Infinix.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi, Afisa wa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa alisema, “MediaTek Helio G80 processor na Teknolojia ya MediaTek HyperEngine Game imeipelekea NOTE 8 kuwa na uwezo wa kuhimili application zenye ujazo mkubwa pasipo simu kupata moto au kuzimika ghafla wakati wa matumizi.”
Karupa alisisitiza, “pamoja kuwa na processor kubwa yenye kukufaidisha wewe mpenzi wa games, kazi nyingi za kiofisi na za shuleni lakini pia Infinix NOTE 8 ina sifa nyingine pendwa kama vile, kamera mbili za mbele zenye MP 16 na kamera 6 nyuma zenye MP 64, chaji yenye kujaza battery ya ujazo wa 5200mAh, kioo cha inch 6.95 na memory ya GB 128Rom kwa GB 6Ram”.
“Umuhimu wa mtandao wenye kasi kwa kila mtumiaji wa smartphone unajulikana, na ili watanzania tusiwe nyuma ya ukuaji wa teknolojia tunahitaji mtandao wenye kasi ili kujifunza mambo mapya kila leo na kwa kulizingatia hilo Vodacom Tanzania PLC inakusogeza karibu na ulimwengu wa kidijital kupitia ofa ya GB 96 katika kila simu ya Infinix NOTE 8 kwa muda wa mwaka mzima,” alisema Nandi.
Infinix na Vodacom Tanzania Plc wamekuwa washirika kwa muda mrefu tangu kuzinduliwa rasmi kwa bidhaa za Infinix nchini. Kampuni hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kuleta mapinduzi katika sekta ya mawasiliano nchini, Simu hii ya Infinix Note 8 inapatikana katika maduka yote ya Vodacom nay ale ya Infinix yaliyopo maeneo yote nchini.
Mwisho….
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment