Migogoro ya Wachimbaji wa Madini inayohusu masuala ya madini haiwezi kutatuliwa kwa matamko ya Baraza la Ardhi kwa kuwa kila sheria inatumika mahala pake. Migogoro ya namna hiyo hutatuliwa kwa kuzingatia kwanza matakwa ya Sheria ya Madini.
Hayo yamesemwa leo Novemba 20, 2020 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila alipotembelea eneo la mgogoro wa wachimbaji wadogo kati ya vikundi vya Wachimbaji wadogo wa Mwime na Isalenge katika mkoa Shinyanga Wilayani Kahama.
Mgogoro huo kati ya vikundi hivyo, uliibuka baada ya vikundi hivyo viwili kutofautiana wakati wakigombea kuteuliwa na Tume ya Madini kusimamia eneo la mlipuko wa madini ya dhahau (gold rush) la Mwime wilayani Kahama.
Katika mchakato wa kumpata atakayepewa jukumu hilo la usimamizi, kamati iliyoteuwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringa Macha ilikipa ushindi kikundi cha Isalenge baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa. Kamati hiyo ilikuwa na makundi mbalimbali kutoka katika ofisi ya wilaya na Ofisi ya Tume ya Madini ya wilaya.
Kutoka na maamuzi hayo Kikundi cha Mwime hakikuridhia Kikundi cha Isalenge kupewa kazi hiyo ndipo walikwenda kushitaki kwenye Baraza la Ardhi la Wilaya. Baraza hilo lilitoa tamko la kutengua maamuzi ya Kamati ya Mkuu wa Wilaya kwa kufuata matakwa ya Sheria ya Ardhi.
“Kamati hii haikuwa na upendeleo. Hoja iliyotumika kukipa ushindi kikundi cha Iselange ni kutoka na kukidhi vigezo vilivyopangwa” alisema Macha.
Baada ya Baraza la Ardhi kutengua maamuzi ya kamati ya Mkuu wa Wilaya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini aliesema maamuzi ya Baraza la Ardhi hayawezi kutatua mgogoro huo kwa sababu sheria za Ardhi haziingiliani na sheria za Madini na kwamba maagizo hayo hayawezi kutekelezwa.
“Baraza la Ardhi halina mamlaka ya kutatua mgogoro wa Wachimbaji wadogo unaohusu masuala ya kimadini. Agizo la Baraza la Ardhi ni batili na halitekelezeki” alisema Prof. Msanjila.
Aliongeza kuwa maamuzi ya kamati ya Mkuu wa Wilaya na maamuzi yake yataendelea kutekelezwa na sio maamuzi ya Baraza la Ardhi.
Akizunguzia baadhi ya wachimbaji wadogo Herman Masamaki alisema mgogoro huo unawapelekea watu kutishiwa maisha na baadhi ya watu ambao wanao onekana kuongeaongea kwa viongozi. Alimuomba Katibu Mkuu kutoa muongozo wa utatuaji wa mgogoro huo.
Mwajuma Ramadhani alisema kuna tatizo juu ya utoaji wa marabaha tunatoa mifuko mitano na mwingine anakuja kutoza tena mifuko mingine.
“Mimi kwakweli sielewi kabisa kunamtu anakuja kutoza mrahaba badae anakuja mwingine anatutoza tena mifuko mingine sasa hapa sielewi” alisema Mwajuma.
Prof. Msanjila alisema kuhusu usimamizi wa mtu au kikundi anaekusanya mapato hapaswi kuwa mtu anaechimba katika eneo hili ndiovyo sheria inavyosema kamati ilizingatia hili katika kuteua.
Kuhusu mrabaha alisema msimamizi hana mamlaka ya kukusanya mapato bali kusimamia eneo la machimbo na kutoa taarifa sahihi kwa mamlaka zinazohusika ili ziweze kufika na kufanya kazi yao. Asiehusika hawapaswi kukusanya mrabaha na hawapaswi kupewa.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment