Jeshi La Polisi Tanzania Na Polisi Msumbiji Kufanya Operesheni Za Pamoja


Mkuu wa wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Msumbiji Bernadino Rafael wamekubaliana kufanya operesheni za pamoja kukabiliana na kikundi cha watu wanaofanya uhalifu katika maeneo ya vijiji vya mpaka unaotenganisha nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo yamefikiwa jana wakati Wakuu hao walipokutana mkoani Mtwara na kufanya kikao kazi cha ujirani mwema baina  ya nchi hizo mbili ambapo wote kwa pamoja wamesema wataendelea kuishirikisha jamii ili kuweza kupata taarifa zitakazosaidia kukomesha mtandao huo wa kihalifu.


from MPEKUZI

Comments