Viongozi wa dini wasisitiza amani uchaguzi mkuu.

Samirah Yusuph
Simiyu. Viongozi wa madhehebu mbali mbali  pamoja na wazee maarufu mkoani Simiyu wamekutana kujadili mwenendo wa amani nchini kuelekea uchaguzi mkuu.

Viongozi hao wakiongozwa na mchungaji Martin Nketo wamekutana wakiwa na dhumuni la kuhamasisha wananchi kupiga kura octoba 28 mwaka huu pamoja kuhawakumbusha umuhimu wa kuilinda na kuitunza amani ikiwa ni pamoja na kurudi nyumbani baada ya kupiga kura ili kusubiri tume ya uchaguzi itangaze mshindi.

Akisisitiza umuhimu wa kuituza amani ambayo ni ngumu kuirejesha iwepo ikipotea mzee Sule Kija alisema amani imeasisiwa tangu wasisi wa nchi hii walipo pigania uhuru hivyo ni wakati wa kupambana kuilinda.

"Waasisi waliacha amani viongozi wote waliotawala waliotawala waliacha amani na sisi tupambane kuhakikisha amani hii haipotei,".

Wakisisitiza kuwa waumini ni miongoni mwa wapiga kura ambao wanatakiwa kuhamasishwa na wao ndio wenye jukumu kubwa kutokana na kuwa wamekuwa wakiwaongoza katika nyumba za ibada hivyo ujumbe utawafikia kwa urahisi zaidi.

Mchungaji Joseph Abel alisema kuwa wakati uliobaki ni ni wa kuwashauri waumini kuweza kujua kuwa wao ni ngao ya amani na wanawajibu wa kulinda amani hiyo.

"Haya makundi yalipo kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi inabidi yatendewe haki, kwa sababu haki ndio msingi wa amani haki ikitendeka amani itasalia amani inaambatana na haki,"  alisema Mchungaji Joseph.

Huku viongozi hao wakitambua uwepo wa watumishi wa Mungu ambao wa wamemezwa na siasa na kusema kuwa viongozi wa dini ni wasuruhishi na wajenzi wa maadili lakini ikiwa kiongozi kaamua kuingia katika siasa asiwagawe waumini.

Akitilia mkazo wa kutenda haki bila kujali itikadi za kidini kwa waumini mchungaji Samwel Matwiga alisema hakuna maana ya matamko yasiyokuwa na tija kwa Taifa kwa sababu yanalenga kuwagawa waumini na kuvuruga dhima ya watumishi kuwa wajenzi wa amani.

Kikao hicho kilimalozika kwa maazimio manne ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kupiga kura pamoja na kuhamasisha wananchi kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na tume ya uchaguzi kwa wapiga kura.


Mwisho.



from MPEKUZI

Comments