Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Yafungua Awamu ya Tatu ya Udahili wa mwaka wa masomo wa 2020/2021

 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufunguliwa kwa Awamu ya Tatu ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2020/2021 kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 4.

Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa amesema, hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya waombaji kukosa udahili na Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (TAHLISO) na baadhi ya Vyuo vyenye nafasi kupeleka maombi ya kuongezeka muda.

Kufunguliwa kwa dirisha la Awamu ya Tatu kunatoa fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kudahiliwa au hawakuweza kuomba udahili katika Awamu mbili zilizopita kutumia nafasi hii ili kupata udahili.

Aidha, amewakumbusha waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Kwanza na wale wa Awamu ya Pili kujithibitisha katika chuo kimojawapo kuanzia sasa.

 



from MPEKUZI

Comments