Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imebaini kuwepo kwa kundi la watu wakiwemo baadhi ya viongozi wa juu wa vyama vya siasa waliojipanga kuharibu taswira ya uchagaguzi kwa kueneza taarifa za uzushi na uongo.
Hayo yalisemwa jana Ijumaa tarehe 23 Oktoba 2020 na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Dk. Mahera alisema “wamejipanga kutafuta na kuweka vielelezo vya uongo na visivyo na uhalisia wakivihusisha na michakato ya uchaguzi huu kwa lengo la kuleta taharuki kwa wadau wa uchaguzi na wananchi kwa ujumla.”
Alisema, miongoni mwa mipango ya kuzusha ni wimbi linaloendelea la kudai kuwapo vituo hewa vya kupigia kura.
Soma taarifa yote ya Dk. Mahera hapa chini;
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment