Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli pamoja na Mkewe Wapiga Kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Idara ya Maji Chamwino, Dodoma

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amefika katika kituo chake cha kupigia kura Chamwino Ikulu na kupiga kura yake mapema asubuhi hii

Akizungumza baada ya kupiga kura, Magufuli amesema; “Napenda niwapongeze wasimamizi wa uchaguzi hapa Chamwino; maandalizi yalikuwa mazuri na watu wamejitokeza kwa wingi, wito wangu kwa Watanzania tujitokeze kwa wingi kupiga kura pia nipende kusisitiza amani.”


from MPEKUZI

Comments