Baada ya Uchaguzi Serikali Kununua Vichwa 39 vya Treni


Rais Magufuli amesema baada ya uchaguzi kukamilika Serikali imejipanga kununua vichwa vya treni 39 kwa njia kuu na vingine 18 vya treni sogeza sogeza.

Mbali na hilo pia imejipanga kununua mebehewa 800 ya kusafirishia mizigo na 37 abiria

Amesema hayo katika uzinduzi rasmi wa treni ya abiria inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Arusha kupitia Moshi na Tanga iliyokuwa imeacha kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 30.

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kutaka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuwa mfano Afrika kwa mashirika yanayofanya biashara na kufanya kazi kwa kuhudumia wananchi wake ikiwemo wanyonge.

Amesema kuna wakati aliwahi kusikia njama za watu wakitaka kuharibu reli hivyo aliwataka Watanzania kulinda miundombinu ya treni inatunzwa ili kuweza kuwasaidia.

“Ujio wa treni hii hapa Arusha, uchumi wake utapanda, watu watafanya biashara, hata mama lishe watapeleka vyakula vyao kwa viongozi wa treni na abiria wanaoteremka, wenye nyumba za kulala wageni watapata wateja kwa mpigo hivyo ujio wa treni hii ni suluhisho kwa ajili ya kujenga uchumi wa maeneo haya,” amesema Magufuli.

Ametumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa Serikali kutokubali kubinafsisha vitu vya msingi katika nchi huku akitolea mfano wa ndege zilizobinafsishwa.



from MPEKUZI

Comments