Mama mzazi wa John Shibuda amuombea kura Dr Magufuli

Na Samirah Yusuph
Maswa
. Mama mzazi wa mgombea wa kiti cha Rais kwa tiketi ya ADA-TADEA Hellena Sandala Fungo, amewaomba wananchi wa wilaya ya Maswa kumchagua mgombea wa CCM John Magufuli ili aendelee kufuta kilio cha wananchi.

Mama Hellena ameyasema Hayo jana alipopewa nafasi ya kuwasalimia wananchi wa wilaya hiyo katika uzinduzi wa kampeni za chama cha ADA TADEA kitaifa katika viwanja vya madecco wilayani hapo mkoani Simiyu.

 Kwa unyenyejevu Hellena alisema anatambua kazi ambao Rais Magufuli amekuwa akizifanya hivyo anawaomba wananchi kabla ya kumchagua mwanaye John Shibuda wamfikilie John Magufuli kwa sababu ni kiongozi aliyeleta mabadiliko yenye manufaa kwa wananchi.

Alisema tangu awali kumekuwa na ndoto ya kupata Kiongozi ambaye atasikiliza kilio cha wananchi na kutekeleza mahitaji yao ambapo mungu kwa upendo wake akamleta Magufuli, hivyo wananchi wamtumie vizuri kwa kumpatia kura.

"Magufuli ni Kulwa,Shibuda ni Dotto ili kazi itendeke vizuri wananchi anzeni na Kulwa kabla ya kumfikilia Dotto kwa sababu Magufuli amefanya mambo mengi mazuri," alisema Mama Hellena.

Ambapo baadhi ya wananchi walieleza namna ambavyo wamempokea John shibuda kugombea kiti cha Rais na kusema kuwa wanamkumbuka kwa miaka Ambayo aliwatumikia katika nafasi ya Ubunge kati ya mwaka 2005 hadi 2015.

"Mchango wake ni mkubwa kipindi akiwa mbuge wa jimbo Maswa akiwa CCM na Maswa Magharibi akiwa Chadema alifanya mengi vile amekuja kuomba tena kuongoza kwa nafasi ya Rais wananchi wataamua wenyewe ni nani wa kumpa kura," alisema Adrian Sungwa mkazi wa maswa.

Akieleza namna ambavyo chama chake kimejikita katika kuhakikisha utawala bora wa kidemocrasia John Shibuda, alisema ADA TADEA imejikita katika kuhakikisha inaleta maendeleo endelevu kwa manufaa ya wananchi.

Shibuda alisema TADEA itasimamia misingi ya utawala bora kwa na kuwa na matumizi mazuri ya rasilimali za nchi ili kuhakikisha kuwa kuna utawala wa nyongeza kwamba wananchi watakapo wachagua wabunge na Rais wa chama hicho watapata kitu kingine cha nyongeza.

Kwa kuzingatia utendaji na uwazi wa serikali kwa kutumia wanasiasa ambao watakuwa wamesoma masomo ya mchepuo wasiasa ili kuondoa wanasiasa wanaoingia katika siasa wakiwa na elimi ya mambo mengine na sio siasa.

Aidha Shibuda alieleza sababu ya kuzindua kampeni katika eneo ambalo aliwahi kuongoza na nimzawa wa eneohilo pia kuwa ni kurudisha heshima Nyumbani ambapo walimuamini kwa miaka mingi licha ya kutokuonekana kwa miaka mitano.

Mwisho.


from MPEKUZI

Comments