Watu Wanne Mbaroni Kwa Tuhuma Za Makosa Ya Kupanga Tukio La Mauaji Ya Mtu Mmoja Jijini Mwanza

Jeshi  La  Polisi  Mkoa  Wa  Mwanza  Linawashikilia  Watu  4  Kwa  Tuhuma  Za  Makosa    Ya Kupanga Tukio  La  Mauaji  Ya  Mtu  Mmoja Wilayani  Ukerewe.

Tarehe 25.08.2020 Majira Ya 02:00hrs Usiku Eneo La Mission, Kata Ya Nyamanga, Kisiwa Cha Ukara, Wilaya Ya Ukerewe, Mkoa Wa Mwanza, Andrew Magai, Miaka 48, Mkara, Mkristo, Mkulima Wa Kijiji Cha Chibasi, Aliuawa Kwa Kupigwa Sehemu Mbalimbali Za Mwili Na Kukatwa Na Vitu Vinavyodaiwa Kuwa Na Ncha Kali Kwa Madai Kuwa Marehemu Kabla Ya Kifo Chake Aliwasafirisha Watu Ambao Hawakutambulika Kwenda Kuvunja Nyumba Ya Magesa Simon @ Wile.

Uchunguzi Wa Awali Umebaini Kuwa Tukio La Kuvunja Nyumbani Kwa Magesa Simon @ Wile Lilikua Ni La Kutengenezwa Ili Kuhalalisha Mauaji Yaliyotokea Eneo Hilo. 

Uchunguzi Wa Kina Unaendelea Ukihusisha Wataalamu Mbalimbali. Mwili Wa Marehemu Ulifanyiwa Uchunguzi Na Daktari Katika Kituo Cha Afya Bwisya Na Kukabidhiwa Kwa Ndugu Kwa Mazishi.

Waliofikishwa Mahakamani Leo 31/08/2020 Ni:-

1.Magesa Simon @ Wile, Miaka 50, Mkala, Mkulima, Mkazi Wa Nyamanga.

2.Makanje Mgeta, Miaka 28, Mkara, Mkazi Wa Kijiji Cha Chibasi.

3.Mkapa Magesa@simon, Miaka 24, Mkara, Mkulima, Nyamanga.

4.Selestini Datusi, Miaka 22, Mkerewe, Mkristo, Mkulima, Nyamanga.

Watuhumiwa Wote Wamefikishwa Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kujibu Tuhuma Zinazowakabili.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawataka Wananchi, Wanasiasa Wa Vyama  Vyote  Kutojiingiza Katika Mambo Ambayo Yanaweza Kuhamasisha Uvunjaji Wa Sheria Na Kuvuruga Amani Na Utulivu Wa Nchi, Limeapa Kuendelea Kuchukua Hatua Kali Kwa Kila Atakayekiuka Sheria.

Imetolewa Na:-
Muliro Jumanne Muliro – Acp
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza
31 August, 2020


from MPEKUZI

Comments