Ronaldinho Aachiliwa Huru Paraguay

Ronaldinho Gaucho ameachiliwa kutoka kifungo cha nyumbani nchini Paraguay baada ya kufungwa kwa kumiliki paspoti ya kugushi.

Staa huyo wa zamani wa vilabu vya PSG, Barcelona na hata AC Milan, alikuwa anashikiliwa na mamlaka  za usalama za Paraguay pamoja na kaka yake ,Roberto de Asas ambaye anatambulika kama meneja wa nyota huyu wa zamani.

Nje ya soka Gaucho anatajwa kama mchezaji anayependa sana anasa na maisha ya ufahari yaliyochangia kutofanikiwa zaidi katika soka  na hata sakata hili la kuingia nchini Paraguay kwa hati ya bandia inaelezwa kuwa walikuwa wanakwenda katika uzinduzi wa moja ya kumbi za starehe ya usiku maarufu kama Cassino.


from MPEKUZI

Comments