Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imezizuia kampuni tatu za ndege kutoka Kenya, ambazo ni Air Kenya Express, Fly 540 na Safarilink Aviation kufanya safari zake nchini kutokana na mvutano unaoendelea baina ya nchi hizo hasa sakata la Covid-19.
Hii imekuja ikiwa ni wiki chache baada ya Kenya kutangaza nchi 130 ambazo wananchi wake wanaruhusiwa kuingia nchini humo bila masharti ya kuwekwa karantini ya siku 14 wakati Watanzania wanaoingia Kenya wakitakiwa kuwekwa karantini.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amethibitisha hilo akisema ndege hizo 3 zimezuiwa kufuatia mgogoro unaoendelea baina ya mataifa hayo.
Wiki iliyopita, Kenya ilitangaza nchi 130 ambazo raia wake wataruhusiwa kuingia bila masharti ya kukaa karantini na Tanzania haikuwepo katika orodha.
Johari amesema zuio la ndege hizo nne halitaondolewa mpaka wasafiri kutoka Tanzania wakijumuishwa kwenye orodha ya raia ambao hawatolazimika kukaa karantini.

from MPEKUZI
Comments
Post a Comment