Mchepuko Aua Mke wa Mtu Baada Ya Kumfumania Na Mchepuko Mwingine

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Derick Dambuve (26), mkazi wa kijiji cha Mgoma wilayani Ngara kwa tuhuma za kuwaua mama na mtoto wake (2), baada ya mtuhumiwa kumfumania mwanamke huyo akifanya tendo la ndoa na Kajere Ibrahim (mchepuko mwingine) nyumbani kwa Derick.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa alifanya unyama huo baada ya kukubaliwa na mama huyo kufanya mapenzi lakini muda mfupi alimkuta akifanya tendo hilo na rafiki yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, alisema jana kuwa wakiwa baa, mtuhumiwa aliwanunulia pombe na baadaye kumuomba rafiki yake aitwaye Alex Kirai ampeleke mama huyo, Helda Amon (28), nyumbani kwake na alimpeleka na kumfikisha salama.

Alisema muda mfupi baada ya kumfikisha na kuondoka alifika rafiki mwingine wa mtuhumiwa aitwaye Kajele Ibrahimu akamtaka kimapenzi akakubali, na wakati wakiendelea kufanya tendo hilo, mtuhumiwa alifika nyumbani kwake na kuwafumania.

"Huyu mama alitoroka nyumbani kwa mume wake kijiji cha Muruvangira na kwenda kijiji cha Mgoma anakoishi mtuhumiwa, kulikuwa na gulio akaamua kwenda baa na ndipo akakutana na mtuhumiwa akamtongoza wakakubaliana wakaanza kunywa pombe.

“Mtuhumiwa ni fundi ujenzi na alikuwa na kazi hajamalizia, akamuomba rafiki yake amsaidie kumpeleka huyo hawara yake nyumbani," alisema.

Kamanda Malimi alisema baada ya kufumaniwa rafiki wa mtuhumiwa alikimbia na ndipo mama huyo alianza kushambuliwa hadi kupoteza maisha na kuwa baada ya mtuhumiwa kumuua mama huyo alimuua pia mtoto wake aitwaye Gladness Amon (2) kwa kumpiga na kifaa cha kufanyia mazoezi.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.



from MPEKUZI

Comments