Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Magharibi mwa Afrika, ECOWAS, na kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Mali wamekubaliana kufunga ukurasa wa enzi za rais aliyepinduliwa madarakani Ibrahim Boubakar Keita (IBK).
Hata hivyo mazungumzo yanatarajia kuendelea kuhusu serikali ya mpito kwa kipindi cha miaka mitatu kama ilivyopendekezwa Agosti 24 na kundi hilo la wanajeshi.
Kundi la wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali tangu walipompindua madarakani rais Ibrahim Boubacar Keita Agosti 18, waataka kuundwa kwa serikali ya mpito ambayo itaongozwa na mwanajeshi na kuongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitatu, kulingana na vyanzo vya ndani kutoka kundi hilo la wanajeshi walio madarakani na ECOWAS.
Taarifa hii imetolewa baada ya saa 48 ya mazungumzo kati ya Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, kupitia ujumbe wake uliokwenda mjini Bamako mwishoni mwa wiki hi iliyopita, na maafisa wa Baraza la Kitaifa la linaloshikilia madarakani nchini Mali.
Vyanzo kutoka kundi la wanajeshi wanaoshikilia madaraka vinabaini kwamba, jeshi linapendekeza kwamba rais awe ni mwanajeshi pamoja na waziri mkuu, huku wengi katika mawaziri wakiwa ni wanajeshi.
Hata hivyo katika makubaliano hayo ni kuwa jeshi limekubali kumuachilia huru rais Ibrahim Boubacar na kurudi nyumbani kwake kuwa tu mtu wa kawaida, kulingana na vyanzo kutoka ECOWAS na kundi la wanajeshi wanaoshikilia madaraka.
Credit:RFI
Credit:RFI
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment