Tundu Lissu Akwama Kuhudhuria Kesi Yake Mahakamani

Kesi ya uchochezi inayomkabili Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu leo Julai 30, 2020, imeahirishwa hadi Agosti 26, baada ya mtuhumiwa kushindwa kufika mahakamani.

Kesi hiyo namba 236 ya mwaka 2017, ilifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es Salaam hii leo Julai 30, 2020, kwa ajili ya kutajwa, mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Cassian Matembele.

Akizungumza Mahakamani hapo Wakili wa Upande wa Utetezi Peter Kibatala amesema kuwa, Lissu hakuweza kufika mahakamani hapo kwa kuwa amejiweka karantini kwa lengo la kujiangalia hali yake ya kiafya, kutokana na yeye kuugua kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Wakili wa Serikali Wankyo Simon, hakuwa na pingamizi katika hilo na kuruhusu ipangwe tarehe nyingine


from MPEKUZI

Comments