Makamu Wa Rais Mhe. Samia Asaini Kitabu Cha Maombolezo Ya Mzee Mkapa...."Taifa Limepoteza Mtu Muhimu"
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassam, ameeleza kufadhaishwa na kifo cha Benjamin Mkapa, Rais wa awamu ya tatu
Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi tarehe 25 Julai 2020, alipofika nyumbani kwa Mkapa, Masaki jijini Dar es Salaam kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.
“Kama kuna jambo kubwa la nchi, akisimama Mkapa basi tunajua suluhi itapatikana. Afrika imepata mshutuo. Kwa hiyo ni kazi ya Mungu, hatuna budi kuipokea.
“Tumepoteza mtu muhimu na sasa kinachofuata baada ya kifo chake ni kufuata fikra zake, mienendo na miongozo yake katika kuiongoza nchi hii,” amesema Mama Samia.
Mkapa amefariki dunia usiku wa kuamkia jana Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 na mwili wake, utazikwa Jumatano tarehe 29 Julai 2020, kijijini kwake Lupaso Mkoa wa Mtwara.
Mkapa amefariki dunia usiku wa kuamkia jana Ijumaa tarehe 24 Julai 2020 na mwili wake, utazikwa Jumatano tarehe 29 Julai 2020, kijijini kwake Lupaso Mkoa wa Mtwara.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment