Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete amesema, jana tarehe 23 Julai 2020 alikwenda kumtembelea Mzee Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu hospitali kabla ya mauti kumfika.
"Kifo ni siri ya Mwenyezi Mungu jana jioni nilikwenda kumuona hospitali, tukazungumza sana, alikuwa na maumivu lakini si maumivu ambayo ukitoka unakuja kuwaambia wenzake eeh huyu mgonjwa, nilivyopata taarifa usiku kama amefariki nikauliza kimetokea nini tena, na nimeondoka nikimuaga kwamba nitakuja tena kesho kukuona , kifo ni siri kubwa maana yake ungekuwa unajua ungeweza kusema hata tunaagana kabisa", amesema Dkt Kikwete.
Dk. Kikwete ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kufika nyumbani kwa Mkapa, Msasaji jijini Dar es Salaam.a letu, Mungu amlaze pema peponi.”
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment