Freeman Mbowe Apita Kura za Maoni Ubunge Hai

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania Chadema Freeman Mbowe ameshinda kura za maoni za kuwani Ubunge wa Hai Mkoa wa Kilimanjaro katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Mbowe amepigiwa kura za maoni jana Jumamosi tarehe 25 Julai 2020 na wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo hilo uliofanyika ukumbi wa KKKT jimboni humo akiwa mgombea pekee wa nafasi hiyo.

 Akitangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo, Michael Kilawaila amesema, Mbowe alipigiwa kura 203 za ndio na mbili za hapana.


from MPEKUZI

Comments