Boti yazama Ziwa Tanganyika, yaua 10

Watu kumi wamekufa maji na wengine themanini na saba wameokolewa baada ya boti kuzama katika ziwa Tangayika.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, – James Manyama amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika  kijiji cha Rufugu wilayani Uvinza na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dhoruba iliyotokana  na upepo mkali katika ziwa Tanganyika na kusababisha boti kupinduka na kuzama.

Aidha Kamanda Manyama amesema kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa boti hiyo ilikuwa na abiria tisini na saba.


from MPEKUZI

Comments