Waziri Kigwangalla Aagiza Kuundwa Kwa Kamati Uanzishwaji Wa Pori La Akiba Na WMA Ya Ziwa Natron.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kuundwa kwa Kamati itakayopitia na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya namna bora ya kushughulikia mgogoro wa uanzishwaji wa Pori la Akiba na WMA ya Ziwa Natron.

Kamati hiyo itahusisha watalaam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wajumbe kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya ya Longido, Ngorongoro,  Monduli na wajumbe kutoka katika vijiji vyenye mgogoro kuzunguka eneo la ziwa Natron.

Dkt. Kigwangalla ameunda Kamati hiyo leo jijini Arusha wakati wa kikao cha kujadili uanzishwaji wa Pori la Akiba na WMA ya Ziwa Natron, kikao kilichowahusisha wawakilishi wa wananchi kutoka kutoka katika maeneo yenye mgogoro wilayani Longido, viongozi wa mila wa kabila la Masai na viongozi wa serikali wa wilaya ya Longido.

Amesema Kamati hiyo itafanya kazi ya kupitia maeneo yote ya vijiji yenye mgogoro na kutoa mapendekezo yatakayoainisha matumizi bora ya ardhi kwa wananchi wanaoishi kuzunguka Ziwa Natron pamoja na kuzingatia maslahi mapana ya Taifa kwa kulinda uhifadhi na ikolojia ya ziwa Natron ambalo ni muhimu duniani kwa mazalia ya ndege aina ya Flamingo.

MWISHO


from MPEKUZI

Comments