Wanahisa wa Benki ya CRDB wameidhinisha gawio la shilingi 17 kwa hisa lililopendekezwa na Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo katika Mkutano Mkuu wa 25 wa Wanahisa uliofanyika kidijitali siku ya jumamosi tarehe 27 Juni, 2020. Wakichangia maoni ya kupitisha pendekezo hilo la ongezeko la gawio kwa asilimia 112.5, Wanahisa wa Benki ya CRDB wamepongeza uongozi na wafanyakazi wa benki hiyo kwa matokeo mazuri yenye tija kwa Wanahisa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay alisema ukuaji wa gawio kwa Wanahisa kutoka shilingi 8 kwa hisa mwaka jana hadi shilingi 17 kwa hisa, umechangiwa na matokeo mazuri ya kifedha ambapo Benki ya CRDB ilipata ongezeko la faida kwa asilimia 87 kufikia shilingi bilioni 120.1 kulinganisha na shilingi bilioni 64 mwaka 2018.
“Matokeo haya yamepelekea Bodi kupendekeza gawio la shilingi 17 kwa hisa ambalo ni historia kwa Benki yetu,” alisema Dkt. Laay hukuaki wapongeza Wanahisa wanahisa kwa kushiriki kwa wingi zaidi katika mkutanon huo uliofanyika kidijitali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay akiwasilisha ripoti yake ya mwaka wa fedha unaoshia Desemba 31, 2019 katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa.
Dkt. Laay alisema mwaka 2019 ulikuwa wa mafanikio kwa Benki ya CRDB na kampuni zake tanzu za Benki ya CRDB Burundi na kampuni tanzu ya Bima.
“Katika kampuni tanzu ya Burundi tumefanikiwa kupata ongezeko la faida la asilimia 146 wakati kwa upande wa kampuni yetu tanzu ya Bima tumefanikiwa kupata ongezeko la faida kwa asilimi 17.”
Aliainisha Dkt. Laay huku akisema kuwa mkakati wa Benki hiyo kupanua wigo wake katika Ukanda wa Afrika ya Mashiriki na Kati unaendelea huku Benki hiyo ikiangazia kupanua wigo katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akiwasilisha taarifa yake katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Ally Laay na kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo.
Akiwasilisha ripoti yake katika Mkutano huo Mkuu wa Wanahisa, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema katika mwaka wa fedha wa 2019 Benki ya CRDB imeshuhudia ukuaji mkubwa katika bishara yake ambapo amana za wateja ziliongezeka kwa asilimia 8 kufikia shilingi trilioni 3.4 kulinganisha na shilingi trilioni 3.1 mwaka 2018, rasilimali ziliongezeka kwa asilimia 11 kufikia shilingi trilioni 6.6 kulinganisha na na shilingi trilioni 5.2 mwaka 2018.
“Tulifanikiwa pia kupanua wigo wa wateja wetu kwa zaidi ya asilimia 50, sasa hivi tuna zaidi ya wateja milioni 3 ukilinganisha na wateja milioni 2 tuliokuwa nao hapo awali,” alisema Nsekela.
“Tulifanikiwa pia kupanua wigo wa wateja wetu kwa zaidi ya asilimia 50, sasa hivi tuna zaidi ya wateja milioni 3 ukilinganisha na wateja milioni 2 tuliokuwa nao hapo awali,” alisema Nsekela.
Nsekela alisema mafanikio hayo ambayo Benki ya CRDB imeyapata yanatokana na jitihada kubwa zilizofanya na Benki hiyo katika kuingiza bidhaa na huduma bunifu na zinaoendana na mahitaji ya wateja katika soko. Mwaka jana Benki ya CRDB iliingiza sokoni huduma ya mikopo ya uwezeshaji kwa wakandarasi na wazabuni ili kusaidia katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali na Sekta.
Huduma nyengine ni pamoja na mikopo ya magari “Safari Car Loan” kwa makampuni ya kitalii, mikopo ya kidijitali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu “Boom Advance” na mikopo ya “Jiwezeshe” maalum kwa ajili ya wamachinga inayotolewa kidijitali kupitia huduma ya SimAccount.

“Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuboresha mifumo yetu ya utoaji huduma kwa njia ya kidijitali. Mwaka jana asilimia 86a ya miamala ya wateja ilifanyika kupitia njia za kidijitali. Hii imetusaidia sana hata pale tulipokumbwa na janga la corona hatukupata tabu ya kuwaambia sana wateja wetu kutumia mifumo hii kwani wengi wo Tayari wanatumia,” alisema Nsekela.
Nsekela alisema Benki ya CRDB pia imeshiriki katika kuboresha na kukuza sekta mbalimbali za maendeleo nchini ikiwa ni pamoja na kusaidia jitihada za Serikali kuiletea nchi Maendeleo kupitia uwekezaji wa miradi mbalimbali ya kimkati ikiwamo mradi wa treni ya mwendokasi (SGR) na mradi wa uzalishaji wa umeme katika bonde la mto Rufiji (Nyerere HydroPower Project). “Tumewekeza pia katika uendelezaji wa sekta ya kilimo, uzalishaji viwandani na miundombinu ya usafirishaji kusaidia kufikia azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa kati unaoshamirishwa na viwanda ifikapo mwaka 2025,” alisema Nsekela.
Afisa Mkuu wa fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo alisema Benki hiyo imeendelea kuimarika zaidi hususani katika upande wa utoaji mikopo huku akibainisha kuwa Benki ya CRDB imefanikiwa kupunguza mikopo chechefu kwa asilimia 35 huku uwiano wa mikopo chechefu ukipungua kutoka asilimia 8.3 hadi kufikia asilimia 5.5. “Kupungua kwa mikopo chechefu kunaakisiwa na mapato yatokanayo na riba ambapo kwa mwaka wa fedha 2019 yaliongezeka kwa asilimia 19 kufiki shilingi bilioni 526,” alisema Nshekanabo.
Wanahisa wa Benki ya CRDB waliipongeza Benki hiyo kwa kuandaa mkutano huo wa Wanahisa kupitia mtandao huku wakisema umekuwa wa mafanikio makubwa sana na kutoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wanahisa, Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye aliupongeza uongozi wa Benki hiyo kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wake Abdulmajid Nsekela akisema wamekuwa wakifanya kazi nzuri kwa maendeleo ya benki, watanzania na taifa kwa ujumla. “Mnastahili pongezi sana, na niipongeze Bodi ya Wakurugenzi kwa kutuchagulia kiongozi kijana na mchapakazi,” alisema Sumaye.

Katika Mkutano huo, Wanahisa wa Benki ya CRDB waliwachagua Prof. Neema Mori na Miranda Mpogolo kuwa Wajumbe huru wa Bodi ya Wakurugenzi, huku Dkt. Edwin Mhede akitambulishwa kama mjumbe mpya wa Bodi akiwakilisha Mfuko wa Uwekezaji wa DANIDA. Wanahisa pia walipiga kura kuidhinisha kampuni ya Ernst & Young kuwa mkaguzi wa nje wa mahesabu kwa mwaka wa fedha 2020.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment