NEC yasubiri tangazo la kuvunjwa kwa bunge ili iweze kutangaza tarehe rasmi ya uchaguzi mkuu.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inasubiri tangazo kwenye gazeti la serikali la kuvunjwa kwa bunge ili iweze kuweka tarehe rasmi ya uchaguzi mkuu.

Mkurugenzi wa NEC, Dkt Wilson Mahera amesema hayo wakato akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na kusema baada ya tangazo hilo tarehe itatangazwa.

Amesema Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kifungu 37(1) kinaielekeza tume kufanya uteuzi kwa wagombea nafasi ya urais, ubunge na udiwani.

Pia, amesema sheria hiyo kifungu cha 46(1) kinaelekeza kuwa tarehe ya uteuzi wa wagombea itatakiwa kutajwa ndani ya siku 60 hadi 90 kabla ya kutangazwa siku ya uchaguzi.


from MPEKUZI

Comments