Mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi Kange, mkoani Tanga anadaiwa kumuua mwanafunzi mwenzake kwa kumchoma kisu baada ya kumkuta kwenye chumba cha rafiki yake wa kike.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi, Blasius Chatanda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kueleza kuwa palitokea ugomvi baina ya wanafunzi wa kiume.
Ugomvi huo ulizuka juzi, baada ya kukutana kwenye chumba cha msichana huyo, huku kila mmoja akiona kuwa ana haki ya kummiliki msichana huyo.
Kwa mujibu wa Kamanda Chatanda, aliyefariki dunia katika tukio hilo ni Athumani Ally Daudi, ambaye anadaiwa alichomwa kisu na Waziri Ramadhan.
Kamanda huyo alisema wanamshikilia binti huyo, huku mtuhumiwa akidaiwa kukimbia.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment