Makada 15 CCM Warejesha Fomu za Kugombea Urais Zanzibar

Wanachama 15 wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamerudisha fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kuzijaza na kudhaminiwa

Hadi jana Ijumaa tarehe 26 Juni 2020, takribani makada 15 kati ya 30 waliojitokeza kugombea nafasi hiyo, walirejesha fomu za kugombea urais wa Zanzibar.
 
Waliorudisha fomu ni, Balozi Ali Abeid Karume, mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume. Dk. Hussein Mwinyi, Waziri wa Ulinzi na Mtoto wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dk. Ali Hassan Mwinyi.

Wengine ni, Shamsi Vuai Nahodha, aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Zanziba. Mhandisi Makame Mbarawa, Waziri wa Maji. Mbwana Bakari Juma, Mbwana Yahya Mwinyi, Omar Shehe Mussa, Mohamed Hijja Mohamed , Mohamed Jumanne ,Issa Suleiman Nassor, Abdulhalim Mohamed Ali, Khamis Mussa Omar, Rashid Ali Juma, Dk. Khalid Salum Mohamed, na Ayoub Mahmoud Mohamed.


from MPEKUZI

Comments