Maalim Seif atangaza kugombea urais Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo

Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Hamad ametangaza kugombea Urais Visiwani Zanzibar kupitia chama chake cha ACT-Wazalendo. 

Amesema, kutokana na imani ya Wazanzibari waliyoionesha katika miaka yote aliyogombea urais wisiwani humo, ameamua kurejea ulingoni kupambana na yeyote atakayepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Amewaomba Wazanzibari kumkubali kama walivyofanya kwa chaguzi zilizopita kwa kuongeza idadi ya wanaompigia kura kila uchaguzi mpya tangu mwaka 1995.

Amesema walifanya tafiti kuona kama wazanzibar kama bado wanamkubali na tafiti hiyo ilionyesha kuwa bado anakubalika ndani ya Zanzibar


from MPEKUZI

Comments