Jamii Yatakiwa kuwafichua wauza dawa za kulevya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameitaka jamii mkoani Tanga kuibua na kuwafichua wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa jengo la huduma za Methadone uliofanyika jijini Tanga.

Amesema jitihada zilizofanywa na serikali mara baada ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) zimesaidia kuthibiti dawa hizo kwa asilimia 90.

Mpaka sasa serikali imezindua vituo nane vya methadone ambavyo ni Muhimbili, Temeke, Mwananyamala, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Pwani na Tanga.


from MPEKUZI

Comments