Wagonjwa wa Corona Kenya Wafika 1888

Watu 143 wamepata maambukizi mapya ya virusi vya corona kulingana na katibu tawala wa wizara ya afya nchini Kenya Rashid Aman.

Idadi hiyo imepelekea wale waliothibitishwa kupata maambukizi hadi hii leo kuwa 1888 baada ya watu 2,959 kupimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Watu 86 kati ya hao ni kutoka Nairobi.

Dkt. Aman pia amesema watu 26 zaidi wamepona na kufisha idadi hiyo kuwa 464.


from MPEKUZI

Comments