Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya Nne (04)

ILIPOISHIA
“Wamesema ni kiasi gani?”   
“Milioni mia sita hamsini, ila nimezungumza nao, hadi kwenye milioni miatano watauza”
“Mage umaipenda hii nyumba”
“Ndio baba ila mbona kodi yao ni garama kiasi hicho?”
“Hapana, jana usiku nilibadilisha mawazo, nikaona nisichukue nyumba ya kupangisha ila ninunue kabisa. Nina imani utaishi kwa amani kabisa kwenye hii nyumba”
Maneno ya nabii Sanga kidogo, yakabakisha kidogo yamuangushe Magreth kwa furaha. Katika maisha yaku hakutarajia hata siku moja kuja kumiliki nyumba ya kwake peke yake, tena nyumba yenye hathi ya mamilioni ya pesa.

ENDELEA
“Au hujapenda mimi kukununulia hii nyumba?”
Nabii Sanga alimuuliza Magreth swali la mtego ikiwa jibu ana lifahamu kwamba ni lazima atahitaji kumiliki nyumba kama hiyo.
“Yaani baba sina hata cha kuzungumza”
“Usijali, hivi ndivyo jinsi Mungu anavyo fungua baraka kwa kila mja wake. Hivyo Mungu amezipitisha baraka zako kupitia mimi”
“Asante sana Mungu na ninazidi kukuombea baba Mungu azidi kukubariki kwenye kila hatua ya huduma yako”
“Nashukuru sana mwanangu”
Tomas akawatembeza kwenye nyumba hiyo yenye vyumba vitatu vya kulala huku vyote vikiwa ni master room na seble mbili za kupumzikia, pamoja na jiko kubwa.
“Kutokana muda umwekwenda, kesho tutakutana na mmiliki wa hii nyumba”
“Sawa baba mchungaji na uzuri ni kwamba hii nyumba ni mpya kabisa, nimali ya shirika moja la ujenzi”
“Ahaa kumbe”
“Ndio kwa hiyo hatununui kwa mbabaishaji, ila tuna nunua kwa shirika ambalo hapo baadaye hawato weza kutudhulumu”
“Ndio maana nina kupenda sana Tomas, huwa una fanya kazi zako kwa uhakika na uaminifu mzuri. Endelea hivyo hivyo, Mungu atazidi kukufungulia milango ya baraka”
“Amen”
Wakarudi ndani ya gari, wakamrudisha Tomas hadi eneo alipo liacha gari lake na kuagana naye.
“Baba mchungaji nina weza kuuliza swali?”
“Uliza tu?”
“Kwa nini una nifanya haya yote kwa wakati mfupi, yaani kuanzia jana nimeona maisha yangu yamebadilika kwa kiasi fulani?”
“Swali zuri sana mwanangu. Unatambua kwenye maisha, hususani haya maisha ya kumcha Mungu, yana changamoto zake na faida zake. Ngoja nikusimulie kisa kidogo ambacho kinahusiana na misha yangu.”
Nabii Sanga alizungumza huku akipunguza mwendo kasi wa gari lake.
“Kipindi nilipo kuwa nina ianza hii hudumua. Nilianza kwenye maisha ya chini sana tena maisha ya ufukara. Watu wengi walinisimanga, ikiwemo ndugu zangu wa tumbo moja. Walidai kwamba nina igiza igiza. Sikumuacha Mungu, na nilikutana na mke wangu, barabarani akishambuliwa na wasichana wezake”
“Akishambuliwa kwa nini alikuwa anashambuliwa?”
“Ahaa alichukua mwanaume wa mtu. Hivyo siku hiyo alikutana na mwenye mume wake. Niliweza kuuamua ugomvi ule huku akiwa amejeruhiwa sana kwa kucha. Hakuwa na sehemu ya kuishia kwa maana huyo mwenye mume wake, aligundua kwamba mume wake ame mpangishia nyumba nzima na alifanya kila analo liweza kuhakikisha ana mfukuza ndani ya hiyo nyumba”
“Basi nilimsaidia na kipindi hicho nilikuwa na kachumba kamoja tu. Takribani miezi tisa tulikuwa tuna ishi kama mtu na dada yake. Niliweza kumbadilisha tabia yake na akwa mcha Mungu kweli kweli. Baada ya kuridhika naye basi nilifanya taratibu zote za kanisa na nikamuoa. Hivyo katika kipindi chote hicho hicho sikuweza kukutana naye kimwili hadi nikamuoa na yeye ndio alikuwa mwanamke wangu wa kwanza kukutana naye kimwili”
“Aiseee!!”
“Yaa. Ona sasa Mungu alivyo kuwa wa ajabu. Mara baada ya kufunga naye ndoa. Huduma yangu ikaanza kutanuka, wadhamini kutoka ndani na nje ya nchi wakazidi kunisaidia. Nikaanza kutajirika taratibu hadi sasa hivi nina utajiri mkubwa sana, ambao hata nikiwaambia wanangu na mimi tisifanye kazi yoyote ya kutuingizia kipato. Basi tunaweza kukaa na pesa niliyo nayo kwa zaidi ya miaka mia moja, tukiwa tuna kula, kunywa na kulala”
“Sasa maana yangu ya kukuadithia wewe hivyo ni ili uweze kujua kwamba Mungu ana makusudi yake kwa kila hatua ya mafanikio kwenye maisha yako. Mimi lango la uchumi lipo kwa mke wangu na wewe lango la uchumi lipo kwa yule Evans aliye lala pale kitandani. Laiti kama asinge kutana na wewe, muda huu usinge kuwemo ndani ya gari langu na wala nisinge jua matatizo yako”
“Ni kweli baba mchungaji”
Magreth alijibu kwa unyonge sana huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake.
“Hivyo weza kutambua makusudi ya kila jambo kwenye maisha yako”
“Amen”
Wakapitia katika hospitali ya Mwanayamala kumjulia hali Evans. Walipo ridhishwa na afya yake, nabii Sanga akamrudisha Magreth nyumbani kwake kisha yeye akaelekea kwake.
‘……….wewe lango la uchumi lipo kwa yule Evans aliye lala pale kitandani. Laiti kama asinge kutana na wewe, muda huu usinge kuwemo ndani ya gari langu na wala nisinge jua matatizo yako’
Maneno ya nabii Sanga yakajirudia akilini mwa Magreth na kujikuta akihisi hali ya tofauti sana kwenye moyo wake. Hali hii hakuwahi kuihisi toka abalehe.
‘Nahisi nina mpenda Evans’
Magreth alizungumza kimya kimya huku akielekea kwa muuza chips katika mtaa huo. Akanunua chipsi mayai na soda.
“Da Mage chupa yangu hukunirudishia”
“Usijali mdogo wangu nitakuletea”
“Fanya hivyo, kesho nitaagizia kreti la soda”
“Sawa miskaki hivi ni bei gani?”
“Mia tano”
“Niwekee miwili”
Japo Magreth ana pesa ya kutosha, ila maisha yake ya kuishi kwa bajeti bado yapo pale pale. Akapita dukani kwa Mangi na kununua daftari kubwa na kalamu, kisha akarudi nyumbani. Akapata chakula hicho cha usiku, kisha akaanza kuandika mipango atakayo ifanya kwenye Mgahawa wake. Alipo hakikisha kwamba bajeti hiyo anayo taka kuanza nayo ime mtosheleza akatamani kumujulisha nabii Sanga muda huo, ila moyo wake ukasita na akajipa matumaini ya kumpatia bajeti hiyo siku inayo fwata.
                            ***
    Gari aina ya Ford Ranger, ikalipita kwa spidi gari la nabii Sanga na kulizuia gari la nabii Sanga kwa mbele. Kitendo hicho kikamfanya nabii Sanga kufunga breki za gafla huku akiwa na wasiwasi mkubwa sana. Wanaume wanne wenye bunduki huku sura zao wakiwa wamezifunika, wakashuka kwenye gari hilo na kumuamrisha kwa ishara nabii Sanga kushuka ndani ya gari hilo.
‘Ehee Mungu ni nini hichi kinacho endelea?’
Nabii Sanga alizungumza huku akifungua mkanda wa siti ya gari lake. Wanaume hao mmoja wao akapiga risasi kwenye kioo cha mbele upande ambao hakuna mtu. Tobo la risasi hiyo likamfanya nabii Sanga kushuka kwenye gari bilia kushurutishwa.
“Jamani kama muna taka pesa chukueni, chukueni tu”
Nabii Sanga alilalama huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga.
“Hatutaki pesa zako na tuna kutaka wewe”
Wakamfunga mikono yake kwa nyuma, kisha wakamfunga kitambaa na kumuigiza kwenye gari lao na kuondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi sana huku wakilitekeleza gari la nabii Sanga eneo hilo. 
Gari hiyo inayo endeshwa kwa mwendo wa kasi sana ikazidi kuchanja Mbuga usiku kwa usiku, huku nabii Sanga akiwa amewekwa chini ya ulinzi mkali sana.
“Jamani nyinyi ni kina nani, mbona mme niteka ikiwa sina uadui na mtu”
Nabii Sanga alilalama, ila kisuku suku alicho pigwa kwenye mbavu za kulia kilimfanya atulie tuli.
“Ukirudia kuuliza swali jingine basi utakufa kabla ya masaa yako”
Gari hilo likafika katika wilaya ya Mkinga. Wakasimamisha gari hilo kwenye moja ya pori ambalo lina nyumba nne tu zilizo jengwa na kikundi cha watekaji wanao fanya kazi zao kwa kulipwa na watu binafsi au makampuni. Wakamshusha nabii Sanga, mzoga mzoga na wakamuingiza kwenye moja ya chumba na kuifunga mikono yake juu na taratibu wakaanza kumvuta na kumfanya nabii Sanga aning’inie hewani, juu asifike wala chini asikanyage.
                            ***
‘Done’
Meseji hiyo ikaufanya moyo wa mrs Sanga kutawaliwa kwa tabasamu pana sana. Akamtazama mfanyakazi wake wa ndani anaye fatilia tamthiia ya kikorea.
“Hivi wewe una jua wanacho kizungumza hao watu?”
“Ndio mama”
“Wewe Rose kweli unataka kuniambia kwamba una jua kikorea? Hembu acha kunitania bwana”
“Najua kidogo kidogo”
“Umejifunzia wapi wewe mtoto?”
“Si kwenye hizi tamthilia. Wakisema jonaaaaa ni sawa sawa na kusema mfalmeeeee”
Maneno ya Rose yakamfanya mrs Sanga kucheka kwa furaha sana. Akaondoka sebleni na kuingia chumbani kwake. Haraka akatoa line iliyopo kwenye simu hiyo, akafungua pochi na kutoa line nyingine ambayo hata mume wake huwa haifahamu wala mwana familia wake yoyote yule. Baada ya kuiingiza line hiyo, akatafuta jina lililo andikwa T.
“Niambie mpenzi wangu”
“Salama, kazi vijana wame ikamilisha”
“Weee eheee imendaje endaje?”
“Mara baada ya mimi na wao kuachana. Nikaanza kuwafuatilia taratubu hadi sehemu aliopo mpeleka msichana yule. Nikawapa vijana ratiba nzima na wamemteka karibu kabisa na hapo kwenu”
“Kazi nzuri Tomas, ndio maana nina kupenda. Mwanaume ana taka kuniletea upuuzi wa kijinga. Hatosheki na mimi hadi anataka  huko nje, ana taka hadi kufungua migahawa na kumnunulia nyumba mtu, haiwezekani kwa kweli”
“Usijali mpenzi wangu, mpango acha uendelee”
“Sawa, ila Tomas ile mechi ya jana mwenzio, unajua nilisahau kuondoka huko kwako hata sija chana nywele”
“Weee ehee ilikuwaje sasa?”
“Huyo mkn** si ndio nikamkuta amekaa sebleni kama kibwengo. Alinitakia tu usiku mwema kisha akenda zake kulala.”
“Usijali mpenzi wangu. Hakikisha kwamba unakuwa makini na hakuna mtu ambaye ana weza kugundua juu ya mahusiano yetu”
“Wala usijali katika hilo. Ila Tomas nina hamu sana na wewe
“Hahaa usijali, kesho ukipata muda kidogo njoo mama”
“Nakupendea hapo. Hakikisha kwamba huyo mpuuzi hajulikani alipo, hadi wiki ijayo”
“Nimekuelewa mke wangu”
“Yaani najisikia vizuri sana unapo niita mke”
“Kweli?”
“Haki ya Mungu vile. Najisikia amani na furaha kabisa.”
“Ehee na kale kabinti vipi nikapoteze?”
“Achana nako, nitapambana naye huku huku kanisani. Nitamuwekea vizingiti hadi ajute ni kwa nini alikaa karibu na mume wangu”
“Sawa mpenzi. Nakupenda sana”
“Nakupenda pia. Mwaaaaa”
Mrs Sanga akakata simu huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana moyoni mwake. Mapenzi yake ya siri na Tomas, dalali wa nabii Sanga, yana miezi saba toka walipo yaanzisha. Tabia mbaya za kufanya mapenzi kinyume na maumbile anazo fanyiwa mrs Sanga na Tomas, zimempagawisha hadi ana jikuta akitamani hata leo mume wake aweze kutoweka duniani.
“Na bado mwaka huu ata koma”
Mrs Sanga alizungumza huku akibadilisha laini hiyo na simu na kuirudisha laini yake halisi. Hazikupita hata dakika mbili simu yake ikaanza kuita. Moyo ukamstuka sana, kwani ni simu kutoka kwa mume wake Mr Sanga. Akaitazama kwa muda simu hiyo kisha akaipokea.
“Ndio mume wangu, upo wapi mbona hurudi nyumbani?”
“Samahani, mimi ni afisa wa polisi kanda maalumu. Ninaitwa ispeka Mussa Rjab. Tumepewa taarifa na wasamaria wema kwamba gari la mume wako limeshambuliwa kwa risasi na hadi ninavyo zungumza hatujajua ni wapi mume wako alipo”
“Ameshambuliwa kwa risasi….Ohooo Mungu waangu, jamani mume wangu”
Mrs Sanga akaanza kujiliza kinafki ila ukweli wa mambo ana utambua kwamba yeye na Tomas wamehusika katika kumteka mume wake.
“Usilie mama, unacho paswa ni kufika hapa eneo la tukio ili kuweza kutusaidia, kwa maana si eneo la mbali sana na hapo nyumbani kwenu.”
“Sawa nina kuja sasa hivi”
Mrs Sanga, akajifunga matenge mawili huku ndani akiwa amevalia suruali na tisheti. Akatoka kwa haraka haraka, akaingia kwenye moja ya gari la familia na kufika eneo la tukio ambalo si mbali na nyumbani kwake. Akakuta polisi pamoja na waandishi wa habari wakiendelea kufanya mahojiano japo kwa baadhi ya watu walio weza kushuhudia tukio hilo.
“Ohoo jamani mume wangu”
Mrs Sanga aliangua kilio huku akishuka ndani ya gari hilo. Askari wawili wa kike waka muwahi iku kumzuia asisogee eneo la tukio.
“Mama tafadhali baki kwenye gari lako. Hili eneo si salama.”
Askari mmoja wa kike alizungumza huku akimshika mrs Sanga mkono.
“Jamani huyo ni mume wangu”
“Ndio ni mume wako ila hapa hayupo kabisa. Jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba una kuwa salama wewe na familia yako. Kama watekaji wamemteka mume wako basi kitakacho fatia hapo ni familia yako.”
Baadhi ya askari pamoja na mkuu wao wakaondoka na mrs Sanga na kuelekea nyumbani kwake.
“Watoto wako wapo wapi?”
“Mmoja yupo chuo. Wawili wapo nje ya nchi”
“Huyu wa chuo, yupo chuo gani?”
“Hapo mlimani”
“Hakikisheni kwamba ana wekewa ulinzi wa kutosha huyo binti”
Mkuu wa kikosi hicho cha polisi alizungumza.
“Sawa mkuu”
“Ikiwezekana akachukuliwe na kuletwa hapa nyumbani”
“Tumekupata mkuu”
“Hembu niambie mume wako ana tatizo japo na mtu au kikundi cha watu?”
“Jamani kama munavyo tambua. Mume wangu ni mtumishi wa Mungu. Hana shida na mtu yoyote, yeye ni mcha Mungu kisawa sawa. Yaani sijui kwa nini wamamteka mume wangu ohooo”
Mrs Sanga alizungumza na kunza kuangua kilio kilicho mfanya mkuu wa kikosi hicho cha polisi kumuacha kwa muda apunguze machungu yake kisha mahojiano yaendelee.
“Mama Sanga, je unaweza hisi kidogo kwa nini watekaji wamemteka mume wako”
“Hapo itakuwa ni pesa tu. Hakuna jengine, oohooo Mungu wangu, ohoo jehova, muokoe mume wangu. Damu ya Yesu kristo, imfunike, wasimfanye jambo lolote baya. Mungu simama naye”
Mrs Sanga alisali maombi ya kinafki na laiti kama mioyo ya binadamu ingekuwa na uwezo wa kuoenaka na bindamu mwengine kwamba ina panga nini juu ya kila tukio. Basi polisi wasinge jisumbua kumuhoji mrs Sanga na siku nyingi sana wangekuwa wamemsweka rumande.
                                ***   
    Katika siku ambazo Magreth amejawa na furaha pamoja hamu ya kupata kile alicho ahidiwa na nabii Sanga ni siku ya leo. Akajiandaa vizuri huku mdomoni mwake, akitawaliwa na mapambio ya kumsifu Mungu. Akaelekea kwenye kituo cha waegesha bajaji huku moyoni mwake akiamini sasa maisha ya kupanda dalala dala yanakwenda kuisha.
“Ila hii nchi sasa imetawaliwa na mambo ya ajabu sana.”
Muendesha bajaji alizungumza huku wakiendelea na safari ya kuelekea hospitali ya Mwananyamala.
“Kwa nini kaka?”
“Kuna watu wana wateka watu na wanavishwa jina .... Yaani nashindwa hata kuelewa, tunaelekea wapi?”
“Nani mwengine ametekwa?”
“Si yule nabii Sanga wa kanisa la Heaven light ministry”
Mapigo ya moyo wa Magreth, yakasimama kwa sekunde kadhaa, kisha yakaanza kumuenda kasi, mwili mzima ukaanza kumtetemeka na jasho likimtiririka usoni mwake, hadi muendesha bajaji akabaki akiwa ameshikwa na butwaa kwa nini hali ya abiria wake imebadilika gafla mara ya kusikia taarifa hiyo.
                                                                                                   ITAENDELEA
Ndoto, matumaini na matarajio ya Magreth sasa yameingia giza. Mwanga alio kuwa akiuhisi mbele ya macho yake sasa umebadilika na kuwa giza nene. Nini kitatokea? Endelea kufatilia kisa hiki cha kusisimua, usikose sehemu ya 05



from MPEKUZI

Comments