Kenya Yaendelea Kurekodi Maambukizi Makubwa Zaidi Ya Wagonjwa Wa Corona

Idadi ya maambukizi ya corona nchini Kenya imefikia watu 1618, hii ni baada ya watu 147 zaidi kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita baada ya sampuli 2831 kufanyiwa uchunguzi.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema  kuwa miongoni mwa maambukizi hayo mapya 147, 90 ni jijini Nairobi na 41 ni huko Mombasa.

Vilevile idadi ya waliofariki imefikia 58 baada ya watu wengine watatu kufariki,wawili huko Mombasa na mmoja huko Kiambu.

Idadi ya waliopona imefikia 421 baada ya watu 13 zaidi kupona na kuondoka hospitalini.


from MPEKUZI

Comments