Bunge Laendelea Kujadili Taarifa Ya LAAC....Mbunge Ashauri Serikali Ianzishe Chuo Cha WIZI

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Bunge la Bajeti  ,mkutano wa 19 kikao cha 38 limeendelea kujadili hoja ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali za Mitaa[LAAC] kuhusu ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali[CAG]  huku serikali ikishauriwa kuanzisha chuo cha Wizi ili kukabiliana na ubadhilifu wa mali za umma.

Wakitoa michango ya maoni  mbalimbali  leo Mei,28,2020 juu ya Ripoti ya CAG iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma na kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa[LAAC],Mbunge wa  Kahama mjini Mhe.Jumanne Kishimba  ameshauri serikali kuanzisha chuo cha Wizi  ili kuweza kupambana na ubadhilifu wa mali za umma.

Mbunge wa Ukerewe Mhe.Joseph Mkundi amesema kuna baadhi ya watumishi ngazi ya halmashauri wasiokuwa waaminifu  wamekuwa wakitumia Mashine za ukusanyaji mapato[POS] kwa njia ya udanganyifu na kusababisha halmashauri kupata hasara hivyo kuna haja ya kuwafukuza huku Mhe.Hasma Mwilima akishauri  namna ya kupata mafunzo Zaidi Wakurugenzi wa halmashauri ili kuweza kupambana na watumishi wasiokuwa waaminifu.

Naibu Waziri wa Kazi ,Ajira na  wenye Ulemavu,Mhe.Stella Alex Ikupa amesema serikali ya awamu ya tano imekuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha mikopo watu wenye ulemavu,huku Naibu waziri Ofisi ya Rais ,utumishi wa Umma na utawala bora Dkt.Mary Mwanjelwa ametoa pongezi kwa watumishi kufanya kazi bila kuchoka  ambapo Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto Godwin Mollel  akizungumzia suala la tiba asilia aemesema  ni suala la kibiblia.

Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.Agelina Mabula amesema wizara hiyo imesogeza huduma za ardhi ngazi ya mikoa huku Naibu Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akizungumzia suala la mapato Zaidi ya Bilioni 17 hazikwenda kwenye miradi ya maendeleo ambapo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Omary Mgumba amekiri hoja ya gharama kubwa katika miradi ya Umwagiliaji.

Akijibu hoja ya posho ya Madiwani,Waziri wa Ofisi ya Rais ,Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI]Seleman Jafo amesema kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni , Zaidi ya Bilioni 10 zimeshalipwa huku     Mwenyekiti wa Kamati ya hesabu za serikali za mitaa [LAAC]  Vedasto Edgar Ngombale akihitimisha hoja ya kamati kwa kuipongeza serikali kwa kuanza kutekeleza maagizo ya CAG.

MWISHO.


from MPEKUZI

Comments