Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kukata uhusiano na Shirika la Afya Duniani WHO, akidai kuwa taasisi hiyo ya kimataifa ni kikaragosi cha China.
Katika kikao na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House jana Ijumaa, Trump alirudia tuhuma zake dhidi ya shirika hilo akidai kwamba linaipendelea China, na eti lilishindwa kushughulikia ipasavyo janga la corona.
Aidha alitumia jukwaa hilo kuituhumu China kwa kusema Dunia inahitaji majibu kutoka kwa China juu ya virusi (vya corona)
Trump amechukua uamuzi huo chini ya wiki mbili baada ya kumuandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunia, Tedros Adhanom Gabrayesus ambapo alidai kuwa, "Marekani itaikatia misaada WHO kikamilifu iwapo haitapiga hatua kubwa za kujiboresha ndani ya siku 30 zijazo."
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment