Wakili Albert Msando Ashikiliwa na Jeshi La Polisi

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Koka Moita, amesema kuwa wanamshikilia Wakili wa kujitegemea Albert Msando, baada ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali juu ya ugonjwa wa COVID-19 kwa madai ya kuwa mkoani humo hali ya maambukizi ni mbaya ili hali yeye hana mamlaka hayo.

Kamanda Moita ameyabainisha hayo leo Aprili 30, 2020, na kusema kuwa Msando alikuwa anaelezea hali mbaya ya ugonjwa wa Corona ndani ya Mkoa wa Arusha kupitia video yake iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, huku akiwataka waandishi wa habari wawe mstari wa mbele katika kutoa taarifa za ugonjwa huo.

"Hali hii ilitoa wakati mgumu kwa wananchi waliokuwa wanasikiliza, kauli hii aliitoa wakati anatoa vifaa vya kujikinga na Corona katika eneo la kaloleni katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, na Serikali ilikwishatoa  maelekezo kuwa mwenye mamlaka ya kutoa tarifa hizo ni Waziri Mkuu, Waziri wa Afya na Mganga Mkuu, hii kauli lazima iheshimiwe" amesema Kamanda Moita.


from MPEKUZI

Comments