Mbaroni Kwa Kurekodi Na Kusambaza Video Zamtoto Akinywa Bia Baa Kwenye Mitandao Ya Kijamii Shinyanga

SALVATORY NTANDU
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linawashikilia Watu watatu kwa tuhuma za kufanya ukatili dhidi ya Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka  (3)na Matumizi mabaya ya Mtandao kwa kumnyesha pombe na kisha kurekodi video na kuirusha kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo Aprili 26 kwa Vyombo vya Habari na Kamanda wa Polisi mkoani humo, ACP Debora Magiligimba imesema kuwa limetokea lilitokea Aprili 24 katika baa itwayo Bondeni huko Mwakitolyo  ambapo watuhumiwa hao walinywesha bia  aina ya Balimi na kurekodi video hiyo kisha kuirusha katika mtandao wa Whatsapp.

Kamanda Magiligimba aliwataja   watu  hao waliohusika na tukio hilo kuwa ni pamoja na   Godius  Novat  katisha (32) baba mzazi wa Mtoto huyu,Irene Alphonce Pima mmiliki wa baa hiyo wote wakazi wa mwakitolyo na Oscar Daniel Makondo (35) mfanyabiashara na mkazi wa Mtaa wa Mayila mjini kahama.

“Baada ya tukio hilo kuripotiwa kikosi Kazi cha askari wa Uhalifu wa Makosa ya Kimtandao kilianza kazi rasmi ya kuwatafuta watuhumiwa hao ambao walifanikiwa kuwakamata Aprili 25 mwaka huu katika Kijiji cha Nyaligongo, Kata ya Mwakitolyo, Wilayani Shinyanga,” alisema Magiligimba.

Ameongeza kuwa baada ya Upelelezi kukamilika Wote kwa Pamoja watafikishwa Mahakamani kujibu Mashitaka yanaowakabili.

Sambamba na hilo Kamanda Magiligimba  alitoa  wito kwa wananchi kuheshimu haki za watoto na kutoa onyo kali kwa  atakayebainika kwenda kinyume hatua kali zitachukiliwa dhidi yake.

Mwisho.


from MPEKUZI

Comments