Idadi ya wagonjwa wa Corona Kenya yafikia 374 baada ya kuripotiwa maambukizi mapya 11

Wizara ya Afya Kenya imesema wagonjwa wengine 11 wa corona wameongezeka leo na kufanya jumla ya visa vya corona kufikia 374.

Taarifa hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Afya Dkt.Rashid Aman ambapo amesema kuwa kati ya maambukizi hayo mapya 11, wawili ni watoto wa miaka mitatu.

Hata hivyo, licha ya maambukizi ya Covid-19 kuongezeka nchini humo,  idadi ya waliopona pia imeongezeka na kufikia 124


from MPEKUZI

Comments