Diamond Akabidhi Kwa Serikali Hoteli Yake Aliyonunua Itumike kama hospitali ya kuhudumia wagonjwa wa corona au kama karantini.
Staa wa muziki nchini Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ametoa ruhusa kwa serikali kuitumia hoteli yake mpya aliyoinunua kama hospitali ya kuhudumia wagonjwa wa corona au kama karantini.
Diamond amesema hayo leo ikiwa ni siku mbili baada kutangaza kuwalipia nyumba watu 500 ili kuondokana na adha ya kodi katika kipindi hiki cha maambukizi ya ugonjwa wa covid-19.
“Misukumo ya kusaidia watu, imetokana na malezi niliyolelewa, maisha niliyotokea na historia yangu ya nyuma. Nikikumbuka shida nilizopitia, napata moyo wa kusaidia wengine.
“Nimenunua hotel maeneo ya Mikocheni B, jijini Dar es Salaam ina vyumba zaidi ya 30, nimeshakabidhiwa documents zangu, ipo kwenye marekebisho kadhaa kisha nitaitambulisha. Kwa sababu sijaanza kui-upgrade, niko radhi niitoe kwa serikali kwa muda huu ili iweze kutumika kama Karantini au Hospital mpaka pale Corona itakapoisha,” amesema Diamond.
Aidha, Mondi amesema hajaweka kiwango cha mwisho cha kodi atakazowalipia wananchi, lakini lazima ataangalia wenye uhitaji haswa. Kwa sababu wapo wanaolipa pesa kubwa mpaka Tsh million 1 kwa mwezi, na mwengine Tsh 60,000 tu na inawashinda.
“Sitaangalia Dar es Salaam peke yake, ntajitahidi na kila mkoa nisaidie walau familia tano. Kwa sababu mikoani pia kuna watu wana shida sana. Sitaangalia jinsia moja zaidi, nitaweka usawa kwa wote. Kwa sababu suala la kodi linamgusa kila mtu, wanawake kwa wanaume.
“Ili kuweza kuwafikia walengwa halisi wanaotakiwa kufaidika na hizi kodi, tutatumia serikali za mitaa. Watu wapo wengi lakini lengo ni kuwafikia masikini, wajane, na wale wasio na uwezo. Baada ya hili la kodi kuisha, nitakuja na mpango wa kuwasaidia Ma-DJ wa ma-club na redio. Kwa sababu ni miongoni mwa kundi lilioathirika sana na kipindi hiki cha Corona,” amesema.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment