TAASISI ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekanusha taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Mamlaka hiyo kusambaratisha mkutano wa Katibu mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa. Kitila Mkumbo na wajumbe wa mkutano mkuu wa Wilaya (CCM) Iramba, Mkoani Singida.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo leo Machi 30 imekanusha na kueleza kuwa taarifa hiyo iliyokuwa ikisambazwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook sio kweli.
Imeelezwa kuwa katika taarifa hiyo iliyosambazwa katika mtandao wa Facebook imeeleza kuwa Profesa. Kitila Mkumbo ambaye ni katibu mkuu Wizara ya maji Machi 20, 2019 aliwaita wajumbe 70 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Wilaya ya Iramba Mkoani Singida ambao pia wanatarajiwa kuwa wapiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchi nzima.
Aidha katika taarifa hiyo iliyosambazwa katika mtandao wa kijamii wa Fcebook imeeleza kuwa katika mkutano huo Prof. Kitila Mkumbo alitoa hongo ya shilingi elfu hamsini kwa kila mjumbe kwa lengo la kuwashawishi ili waweze kumchagua pale muda wa uchaguzi utakapofika na kwamba mkutano huo ulisambaratishwa na TAKUKURU Mkoa wa Singida.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa TAKUKURU Mkoa wa Singida haikushiriki kwa namna yoyote ile katika tukio tajwa na wala haikuwa na taarifa ya uwepo wa kikao kama hicho Machi 29, 2020 katika Wilaya ya Iramba Mkoani Singida na kuwataka wananchi kufahamu kuwa TAKUKURU ni chombo kinachotambua majukumu yake na kinafanya majukumu hayo kwa mujibu wa sheria.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment