Kesi ya mauaji namba 5 ya mwaka 2020 imekuja kutajwa tena kwa Mara ya pili Leo katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Arumeru.
Pichani ni mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya binti wa kazi akiingizwa kwa hakimu mkazi mfawidhi Analia Mushi kutajwa kwa kesi yake huku akijifunika uso gubigubi kama alivyokutwa na kamera ya matukio kwenye mahakama ya wilaya ya Arumeru leo jijini Arusha.Picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha
Sehemu ya umati wa watu waliofuatilia kesi ya Mkami Shrima mshukiwa wa mauaji ya binti wa Kazi Marehemu Salome Zakaria
__________________
Hisia za wakazi wa Jiji la Arusha imewavuta kujazana mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo ambapo mtuhumiwa huyo Mkami Shirima alifikishwa mahakamani hapo kwa usiri mkubwa huku akiwa amejifunika gubigubi na mtandio wa dera.
Kesi hiyo ipo kwa hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Arumeru Analia Mushi ambapo imeelezwa kuwa mshtakiwa Mkami Shirima huko maeneo ya Elkurei mnamo 3 Mwezi March alitenda kosa la kumpiga Mfanyakazi wake wa ndani na kumsababishia kumuua Marehemu Salome Zakaria akijua ni kosa kisheria.
Ilielezwa mahakamani hapo kwamba mnamo tarehe sita mwezi wa tatu huu huko maeneo ya mianzini mtuhimiwa Mkami Shirima alimpiga mfanyakazi wake Salome Zakaria ambaye ni marehemu kwa Sasa akijua ni kosa kisheria.
Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 8 Mwezi wa nne mwaka huu itakapo kuja kutajwa tena na mtuhumiwa amerudishwa rumande gereza kuu la Kisongo.
Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo itakuja kutajwa tena mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Analia Mushi wa mahakama hiyo Mwezi ujao.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment