Mzee Mangula Aanguka Ghafla na Kulazwa ICU.....Rais Magufuli Amjulia Hali

Rais Magufuli leo Jumamosi Februari 29, 2020 amemjulia hali makamu mwenyekiti wa CCM- Bara, Philip Mangula aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kuanguka ghafla jana.

Taarifa ya Mangula kuugua imetolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa huku video zikimuonyesha Magufuli akizungumza naye, baadaye kusali pamoja.

Mangula anaonekana akiwa amelala kitandani huku akiwa na plasta juu ya jicho lake la kushoto.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Mangula ambaye jana alishiriki kikao cha kamati kuu ya chama hicho sambamba na Magufuli kilichofanyika katika ofisi ndogo za CCM zilizopo mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU).

“Mangula aliugua ghafla jana na kisha kukimbizwa hospitali kwa matibabu,” inaeleza taarifa hiyo.

“Utapona na Mungu atakusimamia katika tatizo hili, sisi tulipoona jana umeanguka ilitushtua,” amesema Magufuli na Mangula kujibu, “sijui nimeangukaje.”.


from MPEKUZI

Comments