1. People Daily.
👉Sarah Wairimu, mjane wa mkwasi Muholanzi aliyeuwawa Tob Cohen, ameonyesha kutoridhishwa na hali ya nyumba yake ya Kitisuru.
👉Haya yalijiri mnamo Jumatatu, Januari 27, wakati Wairimu aliruhusiwa kuingia katika makazi yake ambayo imetengwa kama eneo la tukio na DCI, kuchukua virago vyake
👉Wairimu, ambaye alikanusha shtaka la kumuua Cohen alisema atafika mahakamani ili kurejesha umiliki wa nyumba hiyo na kuisafisha.
👉Katika gazeti hili, baadhi ya viongozi wanaomuunga mkono Naibu wa Rais William Ruto wametoa pendekezo kwa serikali ya kuanza kuwalipa vijana ambao hawana ajira.
👉Viongozi hao ambao walikutana mjini Naivasha siku ya Jumatatu, walisema pendekezo hilo linatakiwa kujumuishwa katika ripoti ya BBI ili kuwasaidia vijana kujikimu.
👉Gazeti hili linaripoti kuwa yamkini Wakenya 85 wanaugua virusi vya corona katika mji wa Wuhan nchini China, kulingana na Wizara ya Masuala ya Kigeni.
👉Katika hatua ya kulinda Kenya dhidi ya virusi hivyo, Nairobi imeamuru abiria wote wanaowasili kutoka China kutengwa ili kufanyiwa uchunguzi.
👉Mahakama Kuu imeamuru serikali kujenga vyoo katika barabaru kuu nchini ili kutumiwa na wapita njia.
👉Jaji Kossy Bor alisema ni vyema kwa kila mpita njia kupata nafasi ya kutumia vyoo vilivyo katika hali nzuri, hatua ambayo itawazuia kutumia msitu kujisaidia.
👉Serikali ya Kaunti ya Taita Taveta imefika mahakamani kutaka kupewa amri ya kutumia maji kutoka renchi inayomilikiwa na Naibu wa Rais Ruto.
👉Uongozi wa kaunti hiyo umemkashifu Ruto kwa kugeuza chanzo kuu cha maji ambacho hutumiwa na wakazi wa Wadi ya Mata kuingia katika shamba lake, na kuwaacha wakazi wakitaabika.
Credit:Tuko Kenya
Credit:Tuko Kenya
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment