Serikali Yajiweka Tayari Kukabiliana na NZIGE

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Tanzania inashiriki kusaidia kupoteza nzige walioibuka na kushambulia mashamba nchini Kenya ili wasiongezeke tatizo likawa kubwa zaidi lakini pia lisije likahamia nchini Tanzania.

Majaliwa alisema hayo bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi Januari 30, alipokuwa kijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi aliyetaka kujua namna serikali ilivyojipanga kukabiliana na wadudu hao.

“Hili balaa la nzige ambalo tayari limeshafika katika baadhi ya nchi jirani hasa za Afrika Mashariki, nilikuwa napenda kufahamu, serikali imejipangaje katika kukabiliana na kudhibiti masuala haya,” amehoji.

Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema kuhusu nzige ambao jirani zetu mazao yao yanaharibiwa, ni wadudu hatari ambao wakiingia nchini watamaliza mazao yetu hivyo serikali imemechukua tahadhari ambapo Wizara ya Kilimo inaendelea kuwasiliana na Wizara ya Kilimo nchini Kenya kuona mwenendo na ukuaji wa tatizo hilo.

“Na sisi huku tunajipanga kwa namna ambavyo tunaweza kushiriki kikamilifu lakini serikali yetu inashiriki pia kusaidia nchini kwenye kupoteza wadudu hao ili wasiongezeke tatizo likawa kubwa nchini Kenya lakini pia lisije likahamia nchini kwetu.

“Sasa bado nitoe wito kwa mikoa na wilaya na vijiji vilivyoko mipakani kuwa makini na hao wadudu nzige pale ambapo watawaona wakiingia watoe taarifa haraka sana kwenye mamlaka zao ili hatua kamili zichukliwe,: amesema.


from MPEKUZI

Comments