Rais Magufuli Aliandikia Barua Bunge

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema Rais Magufuli amepokea azimio la pongezi lililofikiwa na Bunge kwenye kikao cha 17, kufuatia mafanikio na mageuzi kwenye utendaji kazi wa Serikali na pia ameandika barua ya kulishukuru Bunge kwa kutambua mchango wake.
 
Barua hiyo ya Rais imesomwa kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 18 na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai  ambapo amesema Rais Magufuli analishukuru Bunge kwa kutambua mchango wake wa kuliletea maendeleo Taifa.

“Niendelee kuwaasa Wabunge na watanzania kwa ujumla tuendelee kuipambania nchi yetu, ili tuweze kufikia maendeleo yenye uchumi wa kati” amesema Spika Ndugai wakati akisoma barua ya Rais Magufuli


from MPEKUZI

Comments