PICHA: Lugola Atoka TAKUKURU, Ahojiwa kwa Masaa 6

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemaliza kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jijini Dodoma, ambapo aliingia saa 1.24 asubuhi na kutoka saa 6.37.

Pamoja na Lugola  wengine wanaotarajiwa kuhojiwa na Takukuru leo ambao wanahusishwa na kashfa  ya mkataba wenye utata  wa  kununua vifaa vya zimamoto na uokoaji vyenye thamani ya Euri 408 (sawa na Sh trilioni moja) kutoka kampuni moja nje ya nchi bila kufuata sheria ni  aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu  , Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni na aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.


from MPEKUZI

Comments