Mtolea Aiomba Serikali Ilifanyie Marekebisho Gereza la Keko Kwa Kuwa Linachukua watu Maarufu

Mbunge wa Temeke (CCM), Abdallah Mtolea ameiomba Serikali  kulifanyia marekebisho gereza la Keko lililoko jijini Dar es Salaam kwa kuwa linachukua watu maarufu wenye kesi kubwa kubwa.

Mtolea ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Januari 29, 2020 wakati akiuliza swali la nyongeza akisema gereza hilo lina upekee kwani hupokea wahalifu wa ‘VIP’.

Amesema licha ya Serikali ya Tanzania kulifanyia marekebisho madogo mwaka 2016, bado kuna tatizo kwa gereza hilo kutiririsha maji machafu katika makazi ya watu hususan kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.


“Gereza la Keko ni VIP limejengwa kwa upekee sana ikilinganishwa na magereza mengine ndio maana huhifadhiwa watu maarufu au wenye kesi kubwa kubwa, je serikali haioni haja sasa ya kulitazama gereza hili kwa jicho lingine ili itenge fedha za kutosha kwaajili ya kufanya ukarabati wa gereza lote,” - Mbunge wa Temeke, Abdalah Mtolea

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Hamad Masauni amekiri gereza hilo linahitaji ukarabati na Serikali itafanya ukarabati wakati bajeti itakaporuhusu.


from MPEKUZI

Comments