Taarifa zinaeleza kuwa mtu mmoja anayeshukiwa kuwa na virusi vya Corona nchini Kenya amepelekwa hospitalini.
Mshukiwa huyo amefikishwa hospitali kuu ya rufaa ya Kenyatta. Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa mtu huyo aliwekwa karantini alipowasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Hapo Jana Kenya iliitahadharisha raia wake kwenda mji wa Wuhan China, mpaka pale mlipuko wa virusi hivyo utakapodhibitiwa.
Wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo ilisema ilikuwa na mawasiliano na raia wake waliokwama katika mji wa Wuhan, mji ambao ni kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo, ambao uko kwenye uangalizi maalum.
''Ubalozi unafahamu kuwa kuna raia wa Kenya 85 mjini Wuhan ambao wamesajiliwa ubalozini hivyo unafuatilia kwa karibu hali hiyo,'' wizara ilieleza kwenye taarifa yake hapo jana.
-BBC
-BBC
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment